Liverpool Yaipa presha Man City, Yaichapa Norwich City 3-1

122

Liverpool imeendelea kutoa presha kwa kinara wa Ligi Kuu England Manchester City kufuatia kupata ushindi wa goli 3-1 dhidi ya timu ya Dean Smith Norwich City mchezo uliopigwa Leo Jumamosi Februari 19, huku ingizo jipya Diaz akifunga goli moja wapo.

Ushindi wa Majogoo wa Jiji la Merseyside unakuwa wa nane mfululizo ingawa kwenye mechi ya Leo walipewa ushindani wa kutosha ambapo hata goli pia walitangulizwa kunako ungwe ya kwanza bao la Milot Rashica.

Hata hivyo, Liverpool waliibuka na kukataa rekodi ya miaka 28 kuvunjwa mbele yao, ambapo Sadio Mane alikuwa wa kwanza kufunga goli kabla ya Mohamed Salah kutupia bao lingine na kisha kijana Luis Diaz mwenye umri wa miaka 25 akifunga bao lake.

Ushindi huo pia unaifanya Liverpool kuwa alama sita pungufu ya kinara Manchester City kabla ya mchezo wa Mabingwa watetezi hao kucheza na Spurs Leo baadaye, Norwich wanaendelea kuwa kwenye wakati mgumu kwenye msimamo wakiwa nafasi ya 20.

Author: Asifiwe Mbembela