Lampard ahusishwa Norwich City

159

Norwich City inaendelea na mazungumzo na aliyewai kuwa kocha wa Chelsea na mchezaji wa klabu hiyo Frank Lampard kurithi mikoba ya kocha Daniel Farke

Mchezaji huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 43, ni miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kuwa kwenye majina yatakayopitishwa klabuni hapo.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna tangazo lolote ambalo limetoka la kumthibitisha kocha huyo ambaye hana kazi tangia kuondoka Chelsea alipodumu miezi 18 akikitumikia kikosi cha The Blues.

Norwich wanakamata nafasi ya hatari kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na alama tano pekee kwenye mechi 11 za Ligi mchezo ujao utakuwa dhidi ya Southamption Novemba 20.

Author: Bruce Amani