City yatinga fainali ya Carabao licha ya kuchapwa na Man United

Mabingwa watetezi wa Kombe la Carabao Manchester City watakutana na Aston Villa kwenye fainali ya kombe hilo, hii inakuja baada ya City kusonga mbele licha ya kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa dimba la Etihad.

City ambao wanafika fainali mara ya tatu mfululizo wameingia fainali hii kwa faida ya magoli waliyoyafunga mchezo wa mkondo wa kwanza 3-1 ambalo jumla ya goli katika michezo miwili iliyocheza inakuwa 3-2 hivyo majirani zao United wanaaga rasmi michuano hiyo.

Wakitafuta goli la kuongoza City walitengeneza nafasi nyingi za wazi licha ya kikwazo kuwa David De Gea ambaye ameokoa michimo mingi langoni mwake.

Goli pekee katika dimba la Etihad limewekwa kimiani na kiungo mkabaji wa Manchester United Nemanja Matic kufuatia mpira uliokufa uliopigwa na Fred dakika chache kabla ya mapumziko, kipindi cha pili Matic alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya mchezo usio wa kiungwana kwa Raheem Sterling.

Matokeo hayo yanaifanya City kukata tiketi ya kucheza dhidi ya Aston Villa mtanange wa fainali utaopigwa dimba Wembley Marchi 1 mwaka huu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends