Dabi ya Jiji la Manchester yamalizika kwa kugawana pointi

400
Mchezo wa Ligi Kuu nchini England kati ya Manchester United wenyeji dhidi ya Manchester City uliochezwa katika dimba la Old Trafford umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya sare tasa ya sufuri sufuri.
Ni mchezo ambao pengine alikuwa anatazamwa zaidi kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer namna ambavyo angekipanga kikosi chake baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig kwa kipigo cha goli 3-2.
Hata hivyo, kasi ya mchezo haikuwa vile ambavyo wengi walikuwa wanakusudia ingawa kipa David de Gea alilazimika kufanya sevu nzuri kwa mpira wa Riyad Mahrez na Rodrigo.
Matokeo ya sare tasa yanaifanya Manchester United kukamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa EPL wakati majirani zao City nafasi ya nane, mtanange wa leo umezikutanishi timu hizo zote zikiwa nje ya nne bora.

Author: Asifiwe Mbembela