Dabi ya Simba, Yanga iko pale pale – Mguto

174

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Steven Mguto amesema mchezo wa dabi baina ya Simba wenyeji na Yanga uliopangwa kufanyika katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Disemba 11, 2021 uko pale pale kama ambavyo umepangwa.

Mguto ametoa kauli hiyo Leo Ijumaa Disemba 11, 2021 baada ya kuwepo kwa sintofahamu na tetesi kuwa huenda mchezo huo ukaota mbawa baada ya kwanza klabu hiyo kugomea kufanya mkutano na Waandishi wa Habari kwa kile kilichoelezwa kuwa moja ya mabango yaliyokuwepo kwenye Ukumbi wa Mikutano kukiuka sheria.

Sintofahamu ya pili ni kuwepo kwa bango la mdhamini mweza wa Ligi GSM uwanjani wakati klabu ya Simba iko nje ya makubaliano hayo.

Pamoja na kuwepo kwa tetesi hizo, Mguto amesema mchezo huo utakuwepo pale pale akisema wao kama Bodi ya Ligi (TPLB) wamekuwa wakitumia busara zaidi kuliko kanuni.

“Sisi tunaamini kwenye busara na kumsikiliza kila mtu kuangalia kama atakuwa na hoja au la, lakini busara tunazingatia”.

Kwa upande wa Simba, kupitia Mwenyekiti wao Murtaza Mangungu amesema wao kama Simba hawako tayari kuweka nembo kwenye jezi yao bila kuwepo kwa makubaliano maalumu.

Dabi ya Dar es Salaam mkondo wa kwanza itachezwa kesho Jumamosi Disemba 11, 2021 kuanzia majira ya saa 11 jioni.

Author: Asifiwe Mbembela