Kikosi cha Ivory Coast Afcon 2022 Cameroon

1,395

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast Patrice Beaumelle ametaja majina ambayo yanaunda kikosi cha timu hiyo kuelekea fainali ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2022.

Majina ambayo yanaunda kikosi hicho ni pamoja na jina la winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha ambaye alizua taharuki katikati ya mwezi uliopita baada ya kuomba kutojumuishwa kwenye kikosi cha kufuzu Kombe la Dunia mwezi Novemba.

Ivory Coast, itaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Afcon 2022 nchini Cameroon hatua ya makundi, katika mchezo wa kundi E kwa kucheza na Equatorial Guinea Januari 12.

Kikosi cha Ivory Coast kiko hivi:

Makipa: Sylvain Gbohouo (Wolkite Ketema, Ethiopia), Badra Ali Sangare (JDR Stars, South Africa), Abdoul Karim Cisse (Asec Mimosas, Ivory Coast), Ira Eliezer Tape (San Pedro, Ivory Coast).

Walinzi: Serge Aurier (Villarreal, Spain), Eric Bailly (Manchester United, England), Willy Boly (Wolverhampton Wanderers, England), Wilfried Kanon (Pyramids, Egypt), Odilon Kossounou (Bayer Leverkusen, Germany), Simon Deli (Adana Demirspor, Turkey), Ghislain Konan (Reims, France).

Viungo: Habib Maiga (Metz, France), Maxwel Cornet (Burnley, England), Serey Die (Sion, Switzerland), Ibrahim Sangare (PSV Eindhoven, Netherlands), Jean-Daniel Akpa Akpro (Lazio, Italy), Franck Kessie (AC Milan, Italy), Hamed Traore and Jeremie Boga (both Sassuolo, Italy), Max Gradel (Sivasspor, Turkey), Jean Michael Seri (Fulham, England).

Na

Washambuliaji: Wilfried Zaha (Crystal Palace, England), Jean Evrard Kouassi (Trabzonspor, Turkey), Nicolas Pepe (Arsenal, England), Sebastien Haller (Ajax, Netherlands), Christian Kouame (Anderlecht, Belgium), Yohan Boli (Al-Rayyan, Qatar), Karim Konate (Asec Mimosas, Ivory Coast).

Author: Bruce Amani