Migne apewa majukumu ya kuinoa Equatorial Guinea

115

Mfaransa Sebastien Migne ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka wa Equatorial Guinea. Kabla ya hapo, Migne alikuwa kocha wa Kenya na kufutwa kazi mwezi Agosti, baada matokeo mabaya wakati wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwezi Julai nchini Misri na mashindano ya CHAN.

Migne atakumbukwa sana nchini Kenya kwa kuiwezesha Harambee Stars kufuzu katika michuano ya AFCON baada ya miaka 15. Hata hivyo, amekabidhiwa mikoba ya Nzalang Nacional, ambayo inaorodheshwa ya 135 duniani katika ubora wa mchezo wa soka na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Mwaka 2015, wakati Equatorial Guinea ilipokuwa mwenyeji wa michuamo ya bara Afrika, ilimaliza katika nafasi ya nne na kupanda hadi katika nafasi ya 49 duniani wakati huo. Kazi kubwa inayomsubiri rais kocha Migne ni kuisaidia timu hiyo kufuzu katika michuano ya matufa bungwa barani Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon.

Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Tanzania, jijini Dar es salaam tarehe Novemba tarehe 11. Mbali na Tanzania, Equitorial Guinea imepangwa pamoja na Tunisia na Libya katika kundi J.

Author: Bruce Amani