Pogba kukaa mkekani hadi Desemba

114

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Paul Pogba huenda akawa nje ya uwanja mpaka mwezi Disemba kwa sababu ya majeraha ya enka aliyoyapata akikitumikia kikosi cha Mashetani Wekundu hao.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ufaransa alijiunga na United kwa mara ya pili akitokea Juventus kwa dau la pauni milioni 89 mwaka 2016 ukiwa usajili wa rekodi, amekuwa nje ya dimba tangu mwezi Septemba.

“Sitegemei kumuona Paul kabla ya mwezi Disemba,” kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer aliwaambia Wanahabari, atakaa nje kwa muda mrefu.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Paul angerejea mapema uwanjani kulingana na maendeleo yake, lakini sasa mambo ni magumu kwa kiungo huyo ambaye amekuwa akitajwa kama mchezaji wa kiwango cha juu.

Majeruhi ya Pogba huenda yakapunguza tetesi za kuhitajika kwa kiungo huyo kwenda katika klabu ya Real Madrid na Paris Saint Germany bila shaka jina la Eriksen.

Author: Bruce Amani