Martial amwaga wino kusalia United hadi 2024

176

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial amesaini mkataba mpya Alhamisi hii, na ataendelea kukipiga na Mashetani hao Wekundu hadi mwaka 2014. Mkataba wa Martial, raia wa Ufaransa pia unaipa United fursa ya kumuongezea mwaka mmoja zaidi, klabu hiyo imesema kuptia kwenye tovuti yake.

Martial mwenyewe amenukuliwa akielezea anavyofurahishwa na kuwa na klabu hiyo. Amesema “ninapenda kumshukuru Ole (Gunnar Solskjaer, meneja wa mpito wa Manchester United), pamoja na timu yake nzima ya ufundi kwa kuniamini na kunisaidia kufikisha katika hatua nyingine kiwango changu cha uchezaji.

Martial alijiunga na Manchester United katika kipindi cha uhamisho cha majira ya joto ya mwaka 2015, akitokea klabu ya Monaco inayoshiriki Ligi 1 ya Ufaransa na amefunga magoli 46 katika michezo 162 akiwa na United. Amefunga mabao 8 katika mechi 18 za ligi hadi wakati huu wa msimu.

“Anthony ni mmoja ya wachezaji mwenye kipaji ambacho kocha yoyote atapenda kufanya naye kazi” amesema kocha Solskjaer alipomzungumzia Martial.

Author: Bruce Amani