Ratiba ya 16 bora, Senegal dhidi ya Uganda

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF limetoa ratiba ya michezo ya hatua ya 16 bora mpaka hatua ya fainali ya michuano ya Kimataifa Afrika Afcon leo Julai 2 baada ya kumalizika kwa michezo ya kundi E na F.

CAF imetoa ratiba hiyo inayoonyesha taifa la Morocco litakuwa la kwanza kucheza mchezo wa ufunguzi katika hatua ya 16 bora dhidi ya Benin saa 17:00 jioni wakati ambao Uganda itacheza dhidi ya Senegal saa 21:00 Julai 5.

Madagascar watavaana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya Ghana kumenyana vikali dhidi ya Tunisia.

Mali itapepetana dhidi ya Ivory Coast huku Algeria ikicheza mchezo wake dhidi ya Guinea.

Nigeria itacheza na bingwa mtetezi Cameroon huku Misri ikichuana vikali dhidi ya vibonde wa michuano hii Afrika Kusini.

Kumbuka kila aya imebeba timu nne kwa maana baada ya michezo ya hatua ya 16 kumalizika, zitaingia hatua ya robo fainali kabla ya kuingia hatua ya nusu fainali, mfano aya ya kwanza Morocco itacheza na Benin-mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi kati ya Uganda na Senegal.

Hatua ya 16 bora inaanza kuchezwa Julai 5 mwaka 2019 ambapo itakuwa Morocco vs Benin saa 17:00.

Wachambuzi wengi kutoka Tanzania wametazama na kuona nchi za Kiarabu kwa maana ya Morocco na Misri zitacheza fainali, hii ni kulingana na ratiba ya michezo na uwezo uliozionyesha timu hizo hatua za awali.

Kwa mpangilio huu nani anaingia fainali, ataingia na nani?

Author: Bruce Amani

Facebook Comments