Tunisia, Mali zasonga mbele Afcon

Tunisia imeungana na Mali kuingia hatua ya 16 bora kutoka Kundi E baada ya kulazimisha sare tasa leo Jumanne Julai 2 dhidi ya Mauritania katika mchezo uliofanyika dimba la Suez.

Sare ya leo kwa Tunisia inakuwa sare ya tatu mfululizo kwa timu hiyo huku ikiwa imejikusanyia alama tatu kwenye michezo hiyo wakati ambapo Mali imeongoza kundi E baada ya kuitandika goli 1-0 Angola katika mchezo uliofanyika dimba la Ismailia na kuongoza kundi hilo.

Matokeo hayo yanaifanya Mauritania na Angola kufungashiwa mizigo kwenye mashindano ya Kimataifa Afrika Afcon 2019 ikiungana na timu nyingine kama Tanzania, Kenya, Burundi, na nyinginezo.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments