Sijawai kupitia ukame wa magoli kama sasa – Werner

386

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Chelsea Timo Werner amesema kuna vitu vingi ambavyo amekuwa akivifanyia mazoezi na kukiri kuwa amepitiwa wakati mgumu wakutofunga goli ambao haijawai kumtokea kama msimu huu.

Werner, ambaye alisajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 53 kutokea RB Leipzig msimu uliopita zilipita mechi 14 za EPL bila kufunga goli kuanzia Novemba hadi Februari.

“Ilikuwa ngumu sana kwangu, kwa sababu kila siku nahitaji kuisaidia timu yangu” alisema mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani.

“Nahitaji kufunga, ni asili yangu, mimi ni mshambuliaji” aliongeza.

Werner, anaweza kuwa sehemu ya kikosi katika mchezo wa leo wa EPL dhidi ya Liverpool, ameshafunga bao tano katika mechi 25.

Author: Bruce Amani