Ubora wa van Dijk ajabu kwa Klopp, mkataba mpya

260

Beki wa kati wa Liverpool Virgil van Dijk ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho mpaka mwaka 2025.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alikuwa na mkataba mpaka mwaka 2023, anafuatia baada ya beki wa kulia Trent Alexander-Arnold, Fabinho na Allison kumwaga wino kutumika ndani ya Majogoo wa Jiji la Merseyside.

Msimu uliopita mchezaji huyo alicheza mechi tano pekee kabla ya kuumia mwezi Octoba ambapo imerejea kuelekea kuanza kwa msimu huu.

Akizungumzia kuongeza mkataba amesema “anafuraha kuwa Liverpool kama ambavyo anafuraha kuongeza kandarasi mpya”.

Akiwa ametumika kwenye mechi 130 za Liverpool, kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp alisema van Dijk ni mchezaji mzuri kiasi kwamba angekuwa anauzwa sasa ingekuwa gharama kumsajili

Author: Bruce Amani