Ushindi wa PSG wapatikana kwa gharama ya kuumia Cavani

142

Walifaulu kupata pointi tatu muhimu katika ligi ya Ufaransa lakini bila shaka ni ushindi ambao ulikuja na gharama yake na utakaomkosesha usingizi kocha Thomas Tuchel hasa kutokana na kibarua kinachomkodolea macho. Mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani huenda akaukosa mtanange wa Jumanne wiki ijayo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 ya Champions League dhidi ya Manchester United baada ya kujiumiza katika ushindi wao dhidi ya Bordeaux.

Mfungaji huyo bora wa PSG alilishika paja lake baada ya kufunga penalty iliyowapa ushindi wa 1 – 0 na nafasi yake ikachukuliwa na Kylian Mbappe. Mshambuliaji mwenza wa Cavani Neymar tayari amewekwa nje ya mechi hiyo ya United kutokana kwa kuwa ni majeruhi. “Inabidi tusubiri. Sina habari nzuri.” Alisema kocha wa PSG Tuchel. PSG sasa wako kileleni na pengo la pointi 13.

Author: Bruce Amani