Beki Eric Bailly ajitia kitanzi Man United hadi 2024

320

Beki wa kati wa Manchester United Eric Bailly ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo utakaomfanya abakie Old Trafford mpaka 2024.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27, raia wa Ivory Coast amecheza mechi 100 tayari tangia ajiunge nayo mwaka 2016 kwa dau la pauni milioni 30.

Hata hivyo, majeruhi ya mara kwa mara yamekuwa kikwazo katika taaluma yake kwa kiasi kikubwa. “Nina furaha kubwa, maamuzi haya sikuhitaji hata kufikiria mara mbili – naipenda Manchester United napendea kuchezea klabu hii”, alisema Eric Bailly.

Kandarasi mpya ina kipengele cha kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Author: Bruce Amani