Benitez awapa matumaini Everton

Kocha mpya wa Everton Rafael Benitez amesema akipata mafanikio klabuni hapo mapema kutanyamazisha kelele za kukosolewa kwake ndani ya klabu hiyo.

 

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 61, amekuwa akikosolewa na mashabiki wa klabu ya Everton kutokana na kauli aliyoitoa mwaka 2007 akiwa Liverpool alisema “Everton ni Timu ndogo”.

 

Upinzani baina ya pande hizo mbili ulipelekea kuwekwa kwa mabango ya kupinga kocha huyo kuteuliwa kuwa kocha ndani ya Toffees.

 

Akizungumza hivi karibuni juu ya kauli ya kuwaita Everton klabu ndogo, amesema “ukiwa kocha wa timu yoyote ile unatakiwa kuitetea kwa nguvu zote katika mazingira yoyote yale”, alisema Benitez.

 

“Kwa maana hiyo, nitafanya kila liwekezanalo kuhakikisha nafanya vizuri hapa Everton kwenye kila mchezo”.

 

“Najua klabu haikufanya vizuri sana msimu uliopita, tunataka kufanya vizuri zaidi ya pale”.

 

Benitez, anachukua nafasi ya Carlo Ancelotti aliyetimukia Real Madrid, anakuwa kocha wa kwanza kufundisha Liverpool na Everton tangia mwaka 1800, alikinoa kikosi cha Liverpool mwaka 2004-2010.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares