Chelsea yampeleka Michy Batshuayi Besiktas kwa mkopo

99

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubeligiji Michy Batshuayi amekubali kujiunga na miamba ya soka la Uturuki, Besiktas kwa mkopo muda mfupi baada ya kuingia mkataba mpya wa kuendelea kusalia Chelsea mpaka 2023.

Michy mwenye umri wa miaka 27, inakuwa mara ya tano kujiunga kwa mkopo na klabu nyingine tangia kusajiliwa klabuni The Blues hapo mwaka 2016.

Batshuayi amewai kutumika ndani ya Borussia Dortmund, Valencia na Crystal Palace mara mbili ambapo alifunga goli 2 kwenye mechi 18 za Ligi. Hajaichezea Chelsea tangia mwaka 2020 mwezi Februari.

Kuondoka kwake kunafuatia ujio wa aliyekuwa mshambuliaji wa Inter Milan na mshambuliaji mweza kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Ubeligiji Romelu Lukaku ambapo pia Tammy Abraham ameondoka na kujiunga na AS Roma ya Jose Mourinho.

Author: Asifiwe Mbembela