Everton yachapwa tena, mashabiki wamzomea Benitez

130

Shida iko pale pale kwa mashabiki wa Everton baada ya kukutana na kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Leo Jumapili Disemba 12, 2021.

Everton ambao wiki iliyopita walishinda mbele ya Arsenal wameshindwa kuendeleza ubora ule ambapo ilishuhudiwa Crystal Palace wakiongoza kwa mabao mawili ya Canor Gallagher akifunga kunako dakika ya 41 na dakika ya 90+3 na bao la tatu likifungwa na James Tomkins dakika ya 62.

Bao pekee kwa Everton limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa West Bromich Albion Solomon Rondon kunako dakika ya 70 likiwa ni bao la kwanza kwa msimu huu.

Matokeo hayo yanaifanya Crystal Palace ambayo ilifungwa bao 1-0 na Manchester United siku nne zilizopita kukwea mpaka nafasi ya 12, wakati mashabiki wa Everton wameendeleza moto wa kumzomea kocha wa timu hiyo Rafael Benitez.

Author: Bruce Amani