Man United Yatoa Kichapo kwa Liverpool

306

Matokeo ya mchezo mzuri ni matokeo bora kwa Manchester United ambayo imeichapa bao 2-1 Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Old Trafford Leo Jumatatu.

Unakuwa ushindi wa kwanza kwa Manchester United kwenye Ligi msimu huu, ukiwa ni ushindi pia wa kwanza kwa kocha ten Hag ambaye alichukua timu mikononi mwa Ole Gunnar Solskjaer kama kocha mkuu.

United walianza kuongoza kwa Jadon Sacho kufunga bao nzuri ambalo lilikuwa na utulivu ndani yake akimalizia pasi ya winga wa Elanga kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu mpaka Marcus Rashford anafungua akaunti ya mabao kwenye Ligi msimu huu akitumia pasi ya Anthony Martial.

Bao la kufutia machozi kwa majogoo wa jiji la Merseyside Liverpool limefungwa na Mohamed Salah kwa kichwa kufuatia makosa katika namna ya kuokoa kwa walinzi wa Manchester United.

Kabla ya mchezo wa Leo, United ilikuwa imecheza mechi mbili za Ligi na kuruhusu kufungwa magoli nane, walifungwa bao 4-1 dhidi ya Brighton kisha 4-0 dhidi ya Brighton.

Author: Asifiwe Mbembela