Mane, Mahrez ndani ya kikosi bora cha Afcon 2019

518
Mashindano ya Afcon 2019 yamefikia tamati Ijumaa ya Julai 19 kwa Algeria kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuifunga Senegal kwa goli 1-0 katika dakika 90 zilizomalizika kwenye dimba la Kimataifa Cairo. Ushindi wa Algeria unakuwa wa pili katika historia ya nchi hiyo baada ya lile la mwaka 1990 zaidi ya miaka 28 sasa.
Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limetaja kikosi bora cha mashindano, kwa maana wachezaji 11 waliofanya vizuri. Ndani ya kikosi hicho wachezaji wa Algeria na Senegal wametawala.
Kikosi chenyewe ni hiki hapa:-
Mlinda Mlango: Rais M’Bolhi (Algeria)
Walinzi: Lamine Gassama (Senegal), Yassine Meriah (Tunisia), Youssouf Sabaly (Senegal), Kalidou Koulibaly (Senegal),
Viungo: Adlene Guediora (Algeria), Idrissa Gana Gueye (Senegal), Ismael Bennacer (Algeria)
Washambuliaji: Riyad Mahrez (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Odion Jude Ighalo (Nigeria)
Kocha amechaguliwa kuwa: Djamel Belmadi (Algeria)

Author: Bruce Amani