Nini kitafanyika kama timu ya England itashinda Europa League

Arsenal na Chelsea zipo katika nusu fainali ya Europa League na ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kubeba kombe hilo mjini Baku, Azerbaijan. Kama mmojawapo atashinda kombe hilo, atafuzu katika hatua ya makundi ya Champions League msimu ujao.

Kama washindi watamaliza nje ya nne bora katika Ligi ya Premier, itaaanisha kuwa timu tano za England zitakuwa katika Champions League.

Hata hivyo, kama watamaliza katika nne bora, basi England haitapata nafasi ya ziada. Timu itakayomaliza ya tatu katika ligi inayoorodheshwa ya tano kwenye viwango vya Uefa, ambayo ni Ufaransa, itatinga hatua ya makundi ya Champions League badala ya kucheza mechi za mchujo.

Hakuna nafasi ya Champions League kwa atakayeshindwa katika fainali ya Europa League.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends