England ikishinda Champions League NA Europa League?

131

Kunaweza kuwa na timu tano tu kutoka nchi moja kwenye Champions League. Hivyo basi, hali hiyo inasababisha mkanganyiko wa kama timu za England zitashinda mashindano yote mawii ya Ulaya na kisha zote zimalize  msimu katika nne bora kwenye ligi.

Hata hivyo, hilo haliwezi kamwe kutokea kwa sasa, kwa sababu Liverpool na Chelsea tayari zina uhakika wa kumaliza katika nne boraa, na Tottenham na Arsenal zinakabiliana

Kama itatokea katika msimu wa usoni, timu ya nne ya Ligi ya Premier haitafuzu katika Champions League na badala yake, itaingia katika hatua ya makundi ya Europa League.

Kutakuwa tu na nafasi mbili za Europa League – kwa timu itakayomaliza ya nne katka Ligi ya Premier na mshindi wa Kombe la FA (au timu ya nafasi ya saba kwenye Ligi ya Premier kama City itashinda Kombe hilo)

Kama itawahi kutokea katika msimu kuwa timu ya England zitashinda Champions League na Europa League – na hakuna yeyote kati yao aliyefuzu kabisa kucheaza Ulaya kwenye ligi hiyo – kutakuwa na timu TISA za Ligi ya Premier zitakazocheza Ulaya (tano katika Champions League na nne katika Europa League)

Kama moja kati yazo itafuzu kucheza Ulaya kupitia ligi kuu na nyingine isiweze, basi kutakuwa na timu tano katika Champions League na tatu katika Europa League.

Author: Bruce Amani