Sikio la kufa halisikii dawa, Paris St-Germain yakutana na kipigo kingine mbele ya wajerumani RB Leipzig

298

Kikosi cha Paris St-Germain kimejikuta kinaduwazwa mbele ya RB Leipzig katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Jumatano hii, ushindi ambao unaifanya Leipzig kufikisha alama sawa na vinara Manchester United katika kundi H.

Angel di Maria aliitanguliza mbele PSG ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligue ya nchini Ufaransa lakini akakosa mechi kabla ya Christopher Nkunku kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Ushindi wa RB Leipzig ambayo mchezo wa mwisho ilikutana na kipigo kizito cha goli 5-0 kutoka kwa United uliletwa na goli la penati iliyongwa na Emil Forsberg.

PSG ambayo ilikuwa bila nyota wao ghali Neymar Jr ilimaliza pungufu kwa wachezaji wawili kufuatia kiungo mkabaji wa zamani wa Everton Idrissa Gueye na beki Presnel Kimpembe kuonyeshwa kadi nyekundu.

Matokeo hayo yanaifanya PSG kuwa na pointi tatu pekee wakati RB Leipzig wana alama sita sawa na Manchester United

Author: Asifiwe Mbembela