Kante aipatia Ufaransa ushindi mbele ya Ureno

Mtanange wa Ligi ya Mataifa Ulaya baina ya Ufaransa na Ureno umemalizika kwa Ufaransa kupata matokeo chanya huku kiungo mkabaji wa Chelsea N’Golo Kante akiwa mfungaji wa goli la ushindi wa 1 – 0.

Ureno ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mataifa wakiwa na staa Cristiano Ronaldo walishindwa kufurukuta mbele ya timu bingwa Kombe la Dunia mwaka 2018 Ufaransa.

Kante, akirudi kwenye kikosi cha kwanza baada ya mechi ya kirafiki ya Finland kuanzia benchi aliipatia timu yake goli pekee na la ushindi ungwe ya pili kunako dakika ya 53.

Author: Asifiwe Mbembela