Mabingwa wa EPL Man City hoi kwa Brighton, wachapwa 3-2

414

Brighton imepata ushindi wa kwanza dhidi ya Manchester City wa bao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Amex Leo Jumanne ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa Brighton tangia mwaka 1989.
Mabingwa hao wapya walianza vyema na kuwanyamazisha takribani mashabiki 7,495 waliojitokeza katika uwanja huo kupitia goli la IIlkay Gundogan aliyemalizia mpira wa winga Riyad Mahrez kabla ya Phil Foden kufunga bao la pili kwa City.
Hata hivyo, baada ya kiungo mkabaji wa Man City Joao Cancelo kuonyeshwa kadi nyekundu, mchezo ulibadilika na wakaanza kushambuliwa kama nyuki.
Ambapo nyota wa zamani wa Genk ya Ubeligiji Leandro Trossard alifunga goli la kwanza na Adam Webster kusawazisha na kabla ya dakika 14 mchezo kumalizika Dan Burn aliingia kambani kwa bao la ushindi, ukiwa wa kwanza kwa miaka 32.
City wanabakia nafasi ya kwanza na alama 83, macho yao Jumapili pamoja na mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea Mei 29, hasa baada ya kuumia kwa kiungo mshambuliaji Ilkay Gundogan.

Author: Asifiwe Mbembela