Mwalimu na mwanafunzi kukutana EPL ni Leeds United ya Bielsa Vs Man City ya Pep Guardiola

347

Wakati mtanange wa Ligi Kuu nchini England kati ya Manchester City dhidi ya Leeds United unategemewa kuchezwa kesho Jumamosi Octoba 3 dimba la Elland Road, moja ya vitu muhimu vya kuviangalia ni pamoja na kukutana kwa mwalimu na mwanafunzi wake.

Kocha Pep Guardiola atasafiri kukutana na Marcelo Bielsa ambapo wawili hao kila mmoja akimuelezea mwezake kama kocha bora, Guardiola anasema “ni kocha bora kumfahamu”.

Licha ya Guardiola kumtaja kocha huyo wa Leeds kama mtu bora bado lijendi wa Kireno Johan Cruyff ni mtu pekee ambaye anamvutia na kuwa kwenye msukumo wa kuwa kama yeye.

Mwaka 2006 baada ya Pep Guardiola kupata kazi ya ukocha wa timu B wa Barcelona kabla ya kuanza kazi, alisafiri hadi Argentina nyumbani kwa Bielsa kupata maoni yake na aprochi nzuri ya kukinoa kikosi chake Barca.

“Pengine ni mtu ambaye navutiwa nae zaidi duniani” alisema Kocha Pep Guardiola.

“Ni meneja bora sana katika namna ya anavyokiongoza kikosi chake. Ni kocha wa kipekee. Hakuna hata mmoja anayeweza kuiga anavyofanya, ni ngumu”.

“Sio kwamba nakutana nae mara kwa mara, lakini kila nikipata muda wa kutosha huwa tunakutana na kuongea mengi, zaidi ya yote ananihamasisha katika kazi yangu”.

Muda mwingine maisha hayako sawa, licha ya heshima na pongezi anazopewa Bielsa hana taji wala tuzo yoyote anayoipokea ngazi kubwa.

Wakati huo Guardiola ameshinda mataji nane ya Ligi, mawili ya Ligi ya Mabingwa na mataji matano ya ndani ya Ligi, mafanikio makubwa kwa Bielsa ni kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kubeba nishani ya dhahabu mwaka 2004 katika mashindano ya Olympics.

Hata hivyo, Guardiola anasema haamini katika tuzo wala mataji kwa kocha ili kuwa bora.

“Thamani ya meneja haitazamwi kwenye kushinda mataji pekee” alisema Pep.

“Timu zangu zimeshinda mataji mengi zaidi ya timu zake lakini akili ya kuusoma mchezo na vitu vingine yuko mbali sana”.

Wakati Guardiola anamtaja Bielsa kama Mwalimu wake na mtu anayevutiwa naye, lakini Bielsa anamtaja Guardiola kama mtu pekee katika mbinu pekee.

“Sifikirii kama mimi ni mwalimu wa Guardiola,” nafikiria Pep yuko katika namna pekee kabisa, kama kuna kocha huru kwenye mbinu zake basi ni Guardiola”.

Je huenda ni kuchezea akili baina ya makocha hao  katika kuelekea mtanange huo, nani kuibuka mshindi pengine muda ukawa hakimu mzuri, Guardiola ametoka kukiongoza kikosi chake kuangukia pua kwa kufungwa goli 5-2 dhidi ya Tottenham wakati Leeds United walipata ushindi wa goli 1-0 kwa Sheffield United.

Author: Bruce Amani