Jepkosgei na Kamworor washinda New York Marathon

102

Mkenya Joyciline Jepkosgei ameshinda mbio za New York marathon kwa upande wa wanawake ikiwa ni mbio zake za kwanza masafa hayo marefu.

Jepkosgei, ambaye ndiye anashikilia rekodi ya mbio za kilomita 10, alishinda New York marathon katika muda wa  saa mbili na dakika 22 na sekunde 38.

Mkenya mwenzake na bingwa mtetezi Mary Keitany, aliyekuwa akilenga ushindi wa tano katika mashindano hayo alimaliza katika nafasi ya pili.

Geoffrey Kamworor, pia kutoka  Kenya, alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume kwa kutumia muda wa 2:08:13, ushindi wake wa pili baada ya ule wa mwaka wa 2017.

Author: Bruce Amani