Leicester yajiwekea mazingira safi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao

78

Leicester City wamejiweka karibu na kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutokea nyuma na kushinda bao 2-1 dhidi ya Crystal Palace, huku Kelechi Iheanacho akiendelea kukiwasha.

Wilfried Zaha aliitanguliza mapema Palace kunako dakika ya 12 akitumia vyema pasi ya Eberechi Eze, Timothy Castagne alisawazisha bao hilo ambalo linakuwa la kwanza kwa kiungo huyo mshambuliaji.

Baadae mshambuliaji wa Kinigeria Kelechi Iheanacho alikwamisha mpira nyavuni kunako ungwe ya pili na kuipa alama tatu Leicester City ushindi ambao unaweka karibu na kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao 2021/22. Ni goli la 12 la msimu kwa Iheanacho.

Matokeo hayo yanaifanya Leicester kubakia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa EPL lakini wajiweka tofauti kwa alama saba dhidi ya timu iliyonafasi ya tano West Ham United, mechi tano zikiwa zimesalia. Mara ya kwanza kwa Leicester kucheza mechi ya Ligi ya Ulaya msimu ujao 2016/17 baada ya msimu nyuma kushinda taji la EPL.

Author: Asifiwe Mbembela