West Bromwich Albion yaungana na Leeds United kupanda Ligi Kuu England

318

West Bromwich Albion wamefanikiwa kurudi EPL kufuatia sare ya goli 2-2 dhidi ya QPR katika mchezo wa mwisho wa msimu wa Ligi daraja la pili – Championship.

Alama moja ya imetosha kuwapandisha ligi kuu huku wakikamata nafasi ya pili nyuma ya vinara Leeds United ambao wiki iliyopita walifanikiwa kujihakikishia kupanda daraja.

Ryan Manning aliitanguliza QPR kabla ya Albion kusawazisha na kuongeza goli la pili kupitia kwa Grady Diangana na Callum Robinson.

Eberechi Eze alitupia goli la pili lenye kuipa alama moja Rangers alama ambayo haikuwazuia West Bromwich Albion kurudi kwa kishindo EPL.

Author: Asifiwe Mbembela