Olimpiki kuendelea licha ya kitisho cha virusi vya corona

Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki, imesema michezo hiyo itaendelea kama ilivyopangwa mwezi Julai, jijini Tokyo nchini Japan, licha ya tishio la virusi vya Corona.

Wanamichezo 11,000 kutoka mataifa 200, wanatarajiwa kushiriki katika michezo hiyo mikubwa duniani.

Hata hivyo, kumekuwa na wasiwasi kutoka kwa mataifa mbalimbali licha ya hakikisho hili, Afrika Kusini, imesema timu yake ya taifa ya soka haitakwenda nchini Japan, mwezi Machi tarehe 27 kucheza mechi ya kirafiki na Japan

Mechi hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika katika uwanja wa Sanga.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends